Friday, 28 October 2016

Jinsi ya kutoa lock simu yoyote ya android

Ni rahisi sana kutoa lock ya aina yoyote kwa simu zenye mfumo wa android OS. Zipo sababu nyingi zinazopelekea mtu kusahau password au pattern aliyoiweka katika simu yake sasa huna haja ya kuwafata mafundi na kupoteza hela zako.. wala huna haja ya kupanik hata kidogo ungana nami katika mada hii kutatua tatizo mwenyewe
Unachotakiwa kufanya katika kufanikisha hili fuata hatua hizi chache tu utakuwa umemaliza kazi

HATUA 1:
Zima simu yako na kutoa betri kwa muda wa dakika kama tano tu arafu rudisha betri katika simu kwasababu unaweza ukaizima simu kumbe imerestart au imesleep ndo mana tunashauri utoe betri na uiache kwa dakika tano kisha uirudishe katika simu yako

HATUA 2:
Simu nyingi za android zinakuwaga na kitufe cha kuwashia, kitufe cha home pamoja na vitufe vya sauti ambavyo ni kupandisha sauti na kushusha sasa unachotakiwa kufanya ni kubonyeza kitufe cha kuongeza sauti na kitufe cha kuwashia pamoja na kitufe cha home (kitufe cha sauti juu + kitufe cha home + kitufe cha kuwashia) kwa muda wa dakika moja au tatu mpaka iwake skilini nyeusi yenye maandishi ya kijani au blue









































HATUA 3:
Hapo utatumia vitufe vya sauti kuchagua na kitufe cha kuwasha kwaajili ya kuiruhusu menyu hiyo menyu kisha chagua wipe data/Factory reset ili kufuta kumbukumbu zote za simu ikiwemo na password,pin au pattern baada ya hapo utasubilia kwa muda ifute vitu vyote mwisho kabisa itawaka yenyewe bila password,pin au pattern

NOTE:
Kwa wale ambao simu zao hazina kitufe cha home mnaweza kutumia 1.kitufe cha kuwasha + kitufe cha sauti juu au 2.kitufe cha kuwasha + kitufe cha sauti juu + kitufe cha sauti chini.... ASANTENI KAMA UMEIPENDA MADA HII AU UNA SWALI NAKURUHUSU UULIZE KATIKA COMMENT NITAKUJIBU

No comments:

Post a Comment

ad 1

Kuhusu

authorNapenda kutumia muda wangu mwingi kuwatatulia watu matatizo walionayo katika teknolojia na mambo mengine mengi.
Soma zaidi →



Matangazo

Tangaza nasi 0656 463 637