Friday, 28 October 2016

Jinsi ya kuondoa virus wanaoficha mafaili katika flash au memory card bila kutumia Antivirus

Naelewa jinsi gani virus wa computer wanavyosumbua watumiaji wa vifaa vya computer kama memory card,flash disk n.k. Kwanza kabisa ningependa kutoa maana ya computer virus na madhara yao wanayoyaleta katika computer na vifaa vyake.
Virus ni programu zinazotengenezwa na watu au makampuni ili ziweze kuharibu programu zingine, pia kuna makundi mengi ya virus ambayo nisingependa kuyazungumzia kwa sasa bali ntaenda kuzungumzia madhara ya virus katika vifaa vya computer kama memory card na flash disk.
Madhara ya virus ni kama yafuatavyo hapo chini:-

  • Virus huaribu programu zingine na kuzifanya zishindwe kufanya kazi kwa ufanisi wake
  • Virus hufuta taarifa muhimu za vifaa vya computer na kuvifanya vishindwe kufanya kazi yake kutokana na taarifa zake za kiprogramu kufutika au kuharibika
  • Virus huweza kuficha na kutengeneza shortcuts za mafaili au programu harisi


je utawezaje kuondoa virus wanaoficha mafaili katika memory card au flash bila kutumia antivirus yoyote?

  • Chomeka flash yako katika kompyuta yako baada ya hapo soma jina la flash yako kama ni C au D au E au F.... kwa mfano flash yangu inasoma F















  • kama unatumia windows xp au windows 7 bonyeza katika start menyu utaona sehemu ya kusearch utaandika cmd au CMD lolote kati ya hilo kisha utaibonyeza hiyo cmd arafu utaona imefunguka na ina rangi nyeusi

















kisha baada ya hapo ukifungua hiyo cmd mbele ya > andika andika maneno yafuatayo attrib -h -r -s /s /d j:\*.* kisha bonyeza enter kumbuka j: hii ni herufi ya flash yako au memory yako kama memory yako inasoma G utaandika attrib -h -r -s /s /d g:\*.* kisha bonyeza enter
baada ya hapo itaload na ikimaliza utaona folder halina jina ndani ya flash yako ukilifungua utaona vitu vyako vyote vilivyopotea. KAMA UNATUMIA WINDOW 8 AU 10 NENDA KATIKA search andika cmd au CMD utaipata hiyo screen nyeusi
KAMA UMEPENDA MADA HII UNAWEZA KUCOMMENT AU KUULIZA SWALI PUNDE NTAKUJIBU........

2 comments:

  1. tukishaandika izo kote katika cmd..then unakuja katika hatua gani

    ReplyDelete
  2. Baada ya kuona hizo docoment zilizopotea hatua inayofata

    ReplyDelete

ad 1

Kuhusu

authorNapenda kutumia muda wangu mwingi kuwatatulia watu matatizo walionayo katika teknolojia na mambo mengine mengi.
Soma zaidi →



Matangazo

Tangaza nasi 0656 463 637